Posts

TOPIC 4: KUTUNGA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

Image
  TOPIC 4:   KUTUNGA KAZI ZA FASIHI ANDISHI UTUNGAJI WA MASHAIRI Utungaji/uandishi wa kubuni ni ule unatokana na hisia ambazo zinamsukuma mtunzi ili atunge kazi yake. Hisia zinaungana na wazo ambapo vitu hivyo vinamsumbua akilini na kumkosesha raha. Mwandishi wa kubuni anataka aliwasilishe wazo lake ili hadhira ifahamu kilichopo moyoni mwake. Mwandishi hukosa usingizi na hivyo hulazimika kuamka na kuandika kile kinachomsukuma akilini mwake. Mambo ya Kuzingatia katika Utungaji wa Mashairi Uandishi wa kubuni unamtaka mtunzi atumie milango yake ya fahamu kinagaubaga. Kuna milango ya fahamu mitano ambayo ni pamoja na: kuona, kunusa, kusikia, kuhisi, na kuonja. 1.   Kuona :  je, mhusika unayemfikiria kichwani mwako unamwonaje? Umbo lake ni la kuvutia au kuchusha? Je, macho yake yakoje – je ni ya golori au la? Ni makubwa au madogo? Je, ni mlemavu wa macho? 2.   Kunusa :  pua zako zinakufanya usikie harufu gani? Je, ni harufu mbaya au nzuri? Je, ni uvundo au maras...

TOPIC 3: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI

Image
  TOPIC 3:   UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI ANDISHI Uhakiki wa Ushairi, Tamthiliya na Riwaya Uhakiki ni kitendo cha kutathmini, kueleza, kuainisha na kutoa maoni juu ya kazi fulani ya fasihi kwa kuongozwa na kaida maalum. Kwa kiwango cha elimu ya sekondari mhakiki anafanya kazi ya uhakiki ili kuonesha mambo yanayojitokeza kama vile, dhamira, migogoro, ujumbe, falsafa, mtazamo, msimamo n.k Dhima ya Mhakiki na Nafasi ya Mhakiki Uhakiki ni kazi ambayo ina mchango mkubwa sana katika kazi za fasihi. Kwa msingi huo uhakiki una dhima zifuatazo: 1. Husaidia wasomaji kuilewa kazi ya fasihi kwa urahisi; Watunzi wa kazi za fasihi hutofautiana katika matumizi ya lugha na taswira, hivyo mhakiki anapofanya kazi ya uhakiki anamsaidia msomaji kuelewa vipengele hivi kwa kuvifafanua kwa lugha rahisi. 2. Husaidia ukuaji wa kazi za fasihi; Mhakiki anapoonesha ubora na udhaifu wa kazi ya mtunzi fulani, watunzi wengine pia watafunguka kifikra na kutunga kazi iliyobora zaidi. 3. Uhakiki hukuza uelewa wa ...