Uundaji wa Maneno
Uundaji wa Maneno Lugha hukua na kubadilika kila wakati kulingana na maendeleo ya jamii. Kigezo kimojawapo cha kukua na kubadilika kwa lugha ni kuongezeka kwa msamiati. Ili msamiati uongezeke katika lugha sharti maneno mapya yaundwe. Njia za Uundaji Maneno Uundaji wa Msamiati hutokea kwa njia mbalimbali zifuatazo: Kubadili mpangilio wa herufi. Kuambatanisha maneno. Kutohoa maneno ya lugha nyingine. Uambishaji wa maneno . Kufanikisha sauti, umbo, mlio na sura. Kuunda msamiati kwa kubadili mpangilio wa herufi Neno hujengwa kwa vitamkwa au herufi. Neno jipya lenye maana tofauti huweza kuundwa kwa kubadili mpangilio wa neno lingine Mfano Neno lima , lina herufi l, i, m, a, herufi hizi huweza kujenga maneno kama mali, kumi,imla, mila. Neno tua lina herufi t, u, a, herufi hizi zina weza kujenga maneno kama:- tatu, tua, viatu, tatua. Njia ya kuambatanisha maneno Kuna njia tatu za kuambatanisha...