Posts

TOPIC 6: UFAHAMU

Image
  TOPIC 6:   UFAHAMU UFAHAMU WA KUSIKILIZA Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe. Kujibu Maswali ya Habari Uliyosikiliza Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha: Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa. Katika ufahamu wa kusikiliza, msikilizaji hana budi kuzingatia mambo yafutayo: 1. Kuwa makini na kuelekeza akili yote kwa mzungumzaji ili kuweza kusikia kila anachokisema. 2. Kutilia maanani vidokezo vya maana ili kubaini iwapo msemaji ana...

TOPIC 5: UANDISHI

Image
  TOPIC 5:   UANDISHI UANDISHI WA INSHA ZA KIADA Insha ni kifungu cha maandishi kilichoandikwa kutokana na mtazamo wa mwandishi katika kujadili juu ya mada fulani. Mwandishi anaweza kuandika kuipinga mada hiyo au kuishadidia mada hiyo. Kuna aina mbili za insha, insha za kaida (zisizo za kisanaa) na insha za kisanaa. Insha za kaida   ni insha zinazotumia lugha ya kawaida kuelezea mambo mbalimbali katika jamii, mfano juu ya mazingira, uchumi, biashara, historia n.k. Muundo wa Insha za Kaida Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na vitu vifuatavyo: 1. Kichwa cha insha ; kichwa cha insha hudokeza kile ulichokijadili katika insha yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k 2. Utangulizi ; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako. 3 . Kiini cha insha ;  katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako...